Bwana ni Mchunga
| Bwana ni Mchunga |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Zaburi |
| Views | 15,229 |
Bwana ni Mchunga Lyrics
- Bwana ni mchunga, sitahitaji.
Majani mabichi, malisho yangu.
Ananinywesha maji matulivu
Atanirudisha nikipotea
- Nipitapo bondeni mwa mauti,
U mlinzi wangu, sitaogopa.
Fimbo lako latosha kunilinda.
Ukinifariji sina hasara.
- Kati ya mateso meza waandaa
Na kikombe changu kinafurika
Umenipaka kichwani mafuta.
Nitaulizaje zaidi kwako.
- Wema na fadhili vinifuate
Siku zangu zote, hata milele.
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana.
Katika ufalme wa pendo lake.