Bwana ni Mchunga Lyrics

BWANA NI MCHUNGA

 1. Bwana ni mchunga, sitahitaji.
  Majani mabichi, malisho yangu.
  Ananinywesha maji matulivu
  Atanirudisha nikipotea
 2. Nipitapo bondeni mwa mauti,
  U mlinzi wangu, sitaogopa.
  Fimbo lako latosha kunilinda.
  Ukinifariji sina hasara.
 3. Kati ya mateso meza waandaa
  Na kikombe changu kinafurika
  Umenipaka kichwani mafuta.
  Nitaulizaje zaidi kwako.
 4. Wema na fadhili vinifuate
  Siku zangu zote, hata milele.
  Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana.
  Katika ufalme wa pendo lake.
Bwana ni Mchunga
CATEGORYZaburi
 • Comments