Bwana ni Mchungaji
Bwana ni Mchungaji |
---|
Performed by | - |
Category | Zaburi |
Composer | Reuben Kagame |
Views | 111,953 |
Bwana ni Mchungaji Lyrics
- Bwana ni mchungaji wangu,
Sitapungukiwa kitu
Hun`laza penye majani mabichi,
Huniongoza kwa maji matulivu
Hakika wema nazo fadhili zitanifuata mimi,
Nitakaa nyumbani mwa Bwana,
Siku zote za maisha yangu
- Hunihuisha nafsi yangu,
Hun`ongoza kwa njia za haki
Nipitapo bondeni mwa mauti,
Sitaogopa wewe u nami
- Gongo lako na fimbo yako,
Vitanifariji mimi
Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu