Heri Hao Walio Kamili

Heri Hao Walio Kamili
Performed by-
CategoryZaburi
Views7,710

Heri Hao Walio Kamili Lyrics

  • Heri hao walio kamili,
    Wafuatao sheria za Bwana, na kutenda yaliyo ya haki
    Heri wenye kumtii Jehova,
    Na kwa moyo watamtafuta, na kufuata hizo njia zake
  • Naam hawakutenda ubatili, wamezifuata hizo njia zake.
    Wewe umetupa mawaidha yako, ili sisi tuyatii yote.
    Ningependa, njia zangu ziwe thabiti.
    Ningependa, Mungu nifuate amri zako,
    Ndipo mimi sitaaibika, nikifuata maagizo yako.
  • Ntakusifu kwa moyo wa unyofu Bwana.
    Nikiisha jifunza hukumu niitatii.
    Nitatii amri, usiniache *2
    Jinsi gani mimi nisafishe njia yangu?
    Ni kwa kutii na kufuata njia yako.
    Moyo wangu umekutafuta Bwana.
    Usiniache nipote mbali.
    Niyaache maagizo yako moyoni.
    Moyo wangu waweka neno lako,
    Ee Bwana, kutenda dhambi sitaki.
  • Neno la Bwana litasimama imara huko mbinguni moyoni.
    Moyo wangu naweka neno lako,
    Ee Bwana Ee Bwana, ninakupa moyo wangu
    Uniokoe niwe wako milele.
  • Nisife na dhambi.
    Ee Bwana ninakupa moyo wangu, unipokee