Mtafuteni Bwana
Mtafuteni Bwana |
---|
Performed by | - |
Category | Zaburi |
Views | 7,512 |
Mtafuteni Bwana Lyrics
(Mtafuteni Bwana) maadamu anapatikana
(Mwiiteni Bwana wenu) Maadamu yu karibu
{Mtu mbaya na aache njia yake ya upotovu,
Asiye haki amrudie Bwana asamehewe } *2
- Bwana Mungu asema mawazo yangu mimi kweli si mawazo yenu,
Wala njia zangu sio njia zenu maana mimi Mungu wenu *2
- Heri wanaozingatia matakwa yake, wamtafutao,
kwa moyo wote, watu wasiotenda uovu wala udhalimu
- Ninakutazama kwa hamu Mungu wangu, mtawala wangu kinga,
nguvu zangu,nitakuhimidi ninapokutegemea
- Angalia mateso yangu niokoe Mungu, unitetee
Mungu nijalie uhai uwe nami daima maana nakutumaini.