Enda Nasi Bwana
Enda Nasi Bwana |
---|
Performed by | - |
Category | Recession |
Composer | Reuben Kagame |
Views | 53,624 |
Enda Nasi Bwana Lyrics
- Tunaomba uwepo wako uende nasi
Ewe Bwana wa majeshi tusikie
Kama huendi nasi, hatuwezi kutoka hapa
Hatuwezi peke yetu, enda nasi
- Tu watu wa shingo ngumu tusamehe
Hatufai mbele zako turehemu
Tusafishe ee Baba, tuonyeshe uso wako
Twahitaji neema yako enda nasi
Tutavua mapambo yetu,
Vitu vyote vya thamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi .
- Tunaomba utuonyeshe njia zako,
Kwa maana umetuita kwa jina lako,
Twalilia ee Bwana, utukufu na uso wako
Bila wewe tutashindwa enda nasi