Enda Nasi Bwana

Enda Nasi Bwana
Choir-
CategoryRecession
ComposerReuben Kagame

Enda Nasi Bwana Lyrics

1. Tunaomba uwepo wako uende nasi
Ewe Bwana wa majeshi tusikie
Kama huendi nasi, hatuwezi kutoka hapa
Hatuwezi peke yetu, enda nasi

2. Tu watu wa shingo ngumu tusamehe
Hatufai mbele zako turehemu
Tusafishe ee Baba, tuonyeshe uso wako
Twahitaji neema yako enda nasi


Tutavua mapambo yetu,
Vitu vyote vya thamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi .


3. Tunaomba utuonyeshe njia zako,
Kwa maana umetuita kwa jina lako,
Twalilia ee Bwana, utukufu na uso wako
Bila wewe tutashindwa enda nasi

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Zaeni Matunda Mema 5814860
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Huniongoza Mwokozi 5814856
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442