Unirehemu Unitakase
| Unirehemu Unitakase | |
|---|---|
| Alt Title | Nitalisifu Nitalihimidi |
| Performed by | - |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | (traditional) |
| Views | 6,384 |
Unirehemu Unitakase Lyrics
- Nitalisifu nilihimidi jina lako Mungu Mkuu.
Nitalitunza nilisujudu kwa wema wako ule mkuuUnirehemu unitakase, mwisho nifike kwako mbinguni.
Unirehemu unitakase, mwisho nifike kwako enzini.
Nitalisifu nilihimidi . . . - Umeyalinda maisha yangu, nayo maovu kaniepusha.
Umenilinda nyumbani mwangu, Baraka zako kwangu ni tele. - Kwenye mabonde hata milima, kaniongoza m-chunga wangu.
Kwenye mashaka na hofu nyingi, kaniepusha we ngome yangu - Nizidishie fadhili zako, kazini mwangu unijalie.
Unifundishe uniwezeshe, nishukuru kwa sala zangu. - Unijalie rehema zako, nitende wema kwa ndugu zangu.
Chuki hasira pia ugomvi, niondolee niwe mpole. - Tukufu kwako ee Mungu Baba, mwana na Roho Mtakatifu.
Ni wewe Alfa pia Omega, mwanzo na mwisho hata milele.
Recorded by St. Paul's Community Choir, Nrb