Ee Mama Yetu Maria

Ee Mama Yetu Maria
ChoirSt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumAsante Mama wa Yesu
CategoryBikira Maria
ComposerP. F. Mwarabu

Ee Mama Yetu Maria Lyrics

{ Ee mama yetu maria,
Twaomba sana ee mama
Usituache gizani kwa mwanao tuombee } *2

 1. Mama yetu Maria, utusikilize
  Sisi wana wako, tunaosumbuka
  Maisha yetu mama, hayana furaha
  Tujaze neema, tupate faraja
 2. Utuombee kwake, mwanao mpendwa
  Atutie nguvu, tushinde maovu
  Dunia ina giza, dunia ni ngumu
  Bila nguvu yake, hatuwezi kitu
 3. Tuombee Maria, tuombee mama
  Ili wana wako, tufike mbinguni