Ishara Kubwa

Ishara Kubwa
Performed bySt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumNakupenda Maria
CategoryBikira Maria
ComposerG. Matui
Views8,497

Ishara Kubwa Lyrics

  1. Ishara kubwa imeonekana Mbinguni *2
    { (Ambapo) mwanamke aliyevikwa jua
    Pia na mwezi chini ya miguu yake
    Na taji la nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake } *2

  2. Tufurahie sote katika Bwana, tunapoadhimisha
    Siku kuu kwa heshima ya Bikira Maria
  3. Jeshi la malaika washangilia, pia wafurahia
    Kupalizwa Mbinguni kwake Bikira Maria
  4. Bwana amefunua wokovu wake, kati ya mataifa
    Ameidhihirisha haki yake juu ya nchi
  5. Atukuzwe Baba pia na Mwana, na Roho Mtakatifu
    Kama mwanzo sasa na siku zote na milele