Kumbuka ee Bikira

Kumbuka ee Bikira
Performed by-
CategoryBikira Maria
Composer(traditional)
Views11,949

Kumbuka ee Bikira Lyrics

  1. Kumbuka, ee Bikira Maria mpole sana
    Haijasikika bado hata mara moja
    Kwamba ulimwacha mtu, aliyekimbilia ulinzi wako
    Aliyeomba msaada na maombezi yako-o
    {kumbuka*3 Eeh Bikira Maria aah }*2
  2. Kwa matumaini hayo, tunakimbilia wewe eh Mama
    Bikira wa mabikira, kwa matumaini hayo
    Tunasimama mbele yako, tukilalamika si wakosefu
    eeh Bikira twaja kwako
    {kumbuka*3 eeh Bikira Maria aah }*2
  3. Eeh Mama wa neno la Mungu, usiyakatae maneno yetu
    Bali upende kuyasikia, Na kuyasikiliza
    {Kumbuka*3 Eeh Bikira Maria aah }*2
Based on the Memoraire