Ewe Malkia Nyota ya Bahari
Ewe Malkia Nyota ya Bahari |
---|
Performed by | - |
Category | Bikira Maria |
Composer | (traditional) |
Views | 4,441 |
Ewe Malkia Nyota ya Bahari Lyrics
- Ewe malkia, nyota ya bahari
U mama mpole mwenye huruma
- Tuombee kwa mwanao, ewe Maria mama yetu mwema
Sisi wanao tunakulilia, tuombee kwa mwanao
Mama mwema msafi kabisa, sikia maombi yetu
{Wafahamu unyonge wetu, hakuna wakumlilia } *2
Mama (wetu) mama wa Mungu msafi
Mama tuombee *2
- Mwenyezi Mungu kamtuma Gabrieli
Mama Maria 'tapata mwana tapata
- Mungu tuma Gabrieli
Maria tapata mwana tapata
- Tamzaa mwana, mwana wa kiume
Naye atakuwa mfalme mkuu
Mwana mwana (wa) kiume
'takuwa mfalme mkuu
- Simjui mume, Maria 'lisema
Ewe malaika niambie 'ambie
Mume, alisema, 'laika niambie
- Roho mtakatifu atakujaza
Nawe utamwita Emmanueli
Ulikubali chukua mimba, chukua mimba,
Na hivyo giza kaondolewa *3
- Maria mama wa Mungu (aaa) Mama tuombee
Mbingu zote za kuheshimu . . .
Mam'etu mwenye usafi . . .
Mam'etu mwenye uzuri . . .
Mam'etu mwenye tukufu . . .