Ewe Malkia Nyota ya Bahari Lyrics

EWE MALKIA NYOTA YA BAHARI

@ (traditional)

 1. Ewe malkia, nyota ya bahari
  U mama mpole mwenye huruma
 2. Tuombee kwa mwanao, ewe Maria mama yetu mwema
  Sisi wanao tunakulilia, tuombee kwa mwanao

  Mama mwema msafi kabisa, sikia maombi yetu
  {Wafahamu unyonge wetu, hakuna wakumlilia } *2

  Mama (wetu) mama wa Mungu msafi
  Mama tuombee *2
 3. Mwenyezi Mungu kamtuma Gabrieli
  Mama Maria 'tapata mwana tapata
 4. Mungu tuma Gabrieli
  Maria tapata mwana tapata
 5. Tamzaa mwana, mwana wa kiume
  Naye atakuwa mfalme mkuu
  Mwana mwana (wa) kiume
  'takuwa mfalme mkuu
 6. Simjui mume, Maria 'lisema
  Ewe malaika niambie 'ambie
  Mume, alisema, 'laika niambie
 7. Roho mtakatifu atakujaza
  Nawe utamwita Emmanueli

  Ulikubali chukua mimba, chukua mimba,
  Na hivyo giza kaondolewa *3
 8. Maria mama wa Mungu (aaa) Mama tuombee
  Mbingu zote za kuheshimu . . .
  Mam'etu mwenye usafi . . .
  Mam'etu mwenye uzuri . . .
  Mam'etu mwenye tukufu . . .
Ewe Malkia Nyota ya Bahari
COMPOSER(traditional)
CATEGORYBikira Maria
 • Comments