Heri Yenu
Heri Yenu |
---|
Performed by | - |
Category | Harusi |
Views | 5,622 |
Heri Yenu Lyrics
Heri yenu Mungu amewaunganisha,
Msitengane mkavunje hili agano.
- Aliumba wazazi wetu kale, paradizoni waitawale.
- Alimwumba Adamu babu yetu, na Eva mzazi wetu wa kwanza.
- Akasema, 'zaeni mkaenee, ijazeni dunia na watu.'
- Leo Mungu amewabarikia, mkafunge agano tukufu.
- Lishikeni agano takatifu, siku zote za maisha yenu.
- Pete yenu kwa kweli, ni muungano waivaayo wasiachane.
- Enendeni wawili tangu leo, miongoni mwa raha na taabu.
- Nyumba yenu ijae upendano, akosaye atubu mapema.
- Na amani ya wenye kumcha Mungu, iwavutie nyoyo za watu.
- Sioni, pendo, subira na heshima, ziwe msingi wa maisha yenu.