Ni Siku Kubwa
| Ni Siku Kubwa |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Harusi |
| Views | 5,054 |
Ni Siku Kubwa Lyrics
- Ni siku kubwa njooni nyote tushangilieni
Kweli kwa shangwe na tupigeni vigelegele
Twaomba Mungu Baba Awabariki awajalie na watoto
- Ni siku kuu ya harusi siku ya furaha
Kwani wawili wamepatana kufunga ndoa
Lindeni ndoa yenu Ili kwa dhiki wala faraja msitengane
- Mungu alipomuumba mwanamume Adamu
Akamuumbia mwanamke waishi pamoja
Agano lake Mungu Msilivumje, msilitupe, mhifadhi.
- Basi wewe mwanamume umpende mke wako
Umlinde na kumtunza asiwe na upweke
Umlinde siku zote Hadi mwenyezi Mungu atakapoamua
- Na wewe mwanamke umpende mume wako tu
Na watoto mtakaojaliwa naye Mungu
Uwatunze kwa wema, na kanisani uwapeleke kwake Mungu