Shangilia Harusi
Shangilia Harusi |
---|
Performed by | - |
Category | Harusi |
Views | 4,024 |
Shangilia Harusi Lyrics
Yelele lele, yelele lele, leo tunayo furaha tele tele
Twasherehekea arusi ya wenzetu
Wamejitolea kwa moyo wao wote
Twasherehekea yote wametimiza
Arusi leo shangilia aa, shangilieni maarusi hawa
Arusi leo furahia aa, furahieni maarusi hawa
- Twaombea baraka zake Bwana
Munapoanza maisha haya mapya
Shetani asiwatenganishe kamwe
Mubaki ndani ya Bwana Mungu wetu
- Ewe mwanaume umpende mke wako
Kwani hiyo ndiyo amri ya Mungu wetu
Nawe mwanamke umpende mume wakao
Ndipo ndoa yenu isimame imara
- Msiwasahau wazazi wenu pia
Kwani hao ndio nguzo ya masha yenu
Watoto wenu na muwatunze vema
Muwapeleke kwa kanisa ya Bwana
- Na sisi sote tulioshuhudia
Arusi yenu siku hii ya leo
Twawahimiza mheshimu ndoa yenu
Kwani ndoa ni sakramenti takatifu
Yelele lele, yelele lele
Shangilieni maharusi hawa, furahieni maharusi hawa