Sikiliza ni Mpendwa Wangu
Sikiliza ni Mpendwa Wangu |
---|
Performed by | - |
Album | Shangwe Shangwe |
Category | Harusi |
Composer | Stanslaus Mujwahuki |
Views | 6,240 |
Sikiliza ni Mpendwa Wangu Lyrics
- Sikiliza ni mpendwa wangu,
Ni mpendwa wangu, tazama anakuja
Sikiliza ni mpendwa wangu,
Ni mpendwa wangu, tazama anakuja
{ Akirukaruka milimani,
Akichacharika vilimani
Mpendwa wangu ni kama paa
Ni kama ayala tazama anakuja } *2
- Tazama tazama asimama
Asimama nyuma ya ukuta wetu
Anachungulia dirishani
Atazama kimiani anakuja
- Mpendwa wangu alinena
Yeye alinena akaniambia
Ondoka ewe mpenzi wangu
Ewe mzuri wangu ili uje zako
- Nitazame nitazame uso wako
Niisikie sauti yako
Maana sauti yako tamu
Ni tamu na uso wako ni mzuri
- Mpendwa wangu kweli ni wangu,
Hakika ni wangu na mimi ni wake
Mpendwa wangu hulisha kundi
Hulisha kundi lake kwenye nyinyoro
- Hata jua lipungue kweli
Na vivuli vyote pia vikimbie
Unigeukie mpendwa wangu
Unigeukie ewe mpendwa wangu