Ee Mungu Wangu Mfalme
| Ee Mungu Wangu Mfalme | |
|---|---|
| Performed by | St. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam |
| Category | Zaburi |
| Views | 6,490 |
Ee Mungu Wangu Mfalme Lyrics
Ee Mungu wangu mfalme nitakutukuza
Nitalihimidi jina lako milele na milele- Bwana ana fadhili ni mwingi wa huruma
Si mwepesi wa hasira ni mwingi wa rehema
Bwana ni mwema kwa watu wote
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote - Bwana kazi zako zote zitakushukuru
Na wacha Mungu wako watakuhimidi
Wataunena utukufu wa ufalme wako
Na kuuhadithia uweza wako - Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake
Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote