Ewe Mama wa Mwokozi
Ewe Mama wa Mwokozi | |
---|---|
Performed by | St. Cecilia Mwenge Dsm |
Album | Usia wa Mama Maria |
Category | Bikira Maria |
Views | 7,392 |
Ewe Mama wa Mwokozi Lyrics
Ewe Mama wa Mwokozi, tusikie wanao
Tunaotoa machozi, kuomba hurumayo
Tuwe wetu muombezi, kwa Yesu mwanao
Maria Mwema tusaidie
Tuwe wetu muombezi, kwa Yesu mwanao
Maria Mwema tusaidie- Utuombee Maria, sisi wana wa dunia
Tunaosongwa sana na maovu - Kwa kuwa wewe ni Mama, Yesu akupenda sana
Atalisikiliza ombi lako - Utuombee kwa Yesu, asafishe dhambi zetu
Ili tupate heri ya milele