Ewe Mama Maria
Ewe Mama Maria | |
---|---|
Performed by | St. Cecilia Mwenge Dsm |
Album | Nakupenda Maria |
Category | Bikira Maria |
Composer | P. F. Mwarabu |
Views | 19,092 |
Ewe Mama Maria Lyrics
Ewe mama Maria, mama yetu mwema, Mama wa Mungu
Sisi wanao leo, tunakusalimu, salamu Mama- Ee mama yetu mwema, mama yetu Maria
Sisi tunakupenda tunakupenda sana - Ee mama yetu mpenzi, sikia ombi letu,
Katika shida zetu, kwa mwanao tuombee - Ee Mama mbarikiwa, mama msafi wa moyo
Mama mwenye huruma, uwe nasi daima - Na mwisho mama wa ugeni huu,
Tusaidie Mama, tufike juu Mbinguni