Nimemwacha Wapi Bwana
Nimemwacha Wapi Bwana |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Composer | E. A. Minja |
Views | 6,849 |
Nimemwacha Wapi Bwana Lyrics
- Mimi ni kitu gani na niko wapi, ninatoka wapi
Ninakwenda wapi, mimi nimemwacha Bwana wangu nimtumainiaye
Kaniumba kanitofautisha na wanyama kwa utashi
Ndiye anayeitegemeza nafsi yangu mchana usiku hunilinda
{Nimemwacha wapi (Bwana) Bwana wangu
mimi naenda kujiongoza
Imani yangu imekuwa nia tu siku hadi siku
Matendo yangu yamekuwa ni kinyume toka kitambo
Kwa ajili hii ona ninafanya kazi
na kujinyima nafsi yangu mema } *2
- Maisha yangu ni safari tangu kuumbwa kuzaliwa
Na kuishi kwangu hapa duniani mwisho nipate uzima wa milele
Yeye anipaye pumzi ya uhai wangu na mlinzi wa maisha yangu
Kwa kila hatua ya maisha yangu hapa duniani
- Kanisani nakwenda natoa sadaka na zaka
Lakini ulevi mimi unanitawala kwani pombe ndiye wangu mfariji
Anasani maishani yake na ya famili yake
Na gizani uzinzi ni wangu rafiki sakramenti ya ndoa iko wapi
- Watoto wapatao mali kwa mganga kupiga bao
Nyumba nayo izindikwe hirizi, mikononi nami urogi kaurithi
Kutosita hio nihoji ndugu na jirani
Ati jirani yule ndiye jina fulani nikimsema kusengenya napenda
- Maana sheria zako ni kama kioo mbele ya matendo yangu,
Moyo wangu wanielemea nikitafakari matendo yako
Maana sheria zako ni kama kioo mbele ya imani yangu,
Maisha yangu yamekuwa gizani tena ni maisha ya dhambi
- Ewe ndugu yangu jiulize moyo wako uko wapi
Na matendo yako yampendeza Muumba wako kwa uzima alokupa
Ewe Baba mama vijana ewe mlei hebu jiulize
Mwisho wa maisha yako haya utaupata uzima wa milele