Uzuri wa Kifo

Uzuri wa Kifo
Performed byKwaya ya Malkia wa Mitume Parokia ya Vincent Palloti Arusha
AlbumDira
CategoryMazishi
ComposerBernard Mukasa
Views5,833

Uzuri wa Kifo Lyrics

  1. Basi ndugu zangu, hatimaye imetosha
    Acheni kunung'unika kuhusu kifo
    Jitayarisheni ili mfe kifo chema
    Hiyo hekima ya kweli na ucha Mungu kamili
    Kifo ni zawadi ya upendo toka kwa Mungu
    Nacho kimeandaliwa kuivuka dunia chungu
    Ibada na dini zenu ni upuuzi mtupu
    Kama mwisho wake siyo kumfikia Mungu
    Lakini hamuwezi kumfikia Mungu
    Isipokuwa kwa njia hii ya kifo

  2. Dhambi ya Adamu ilimfanya Adamu,
    akajificha mbali na uso wa Mungu
    Akapewa kifo,
    kusudi roho yake irudi karibu na Mungu milele
  3. Kifo kilibeba maana yake halisi,
    alipoinuliwa Mwokozi wa watu
    Akashinda kifo,
    kusudi watu wake baada ya kifo warudi kwa Mungu
  4. Kama hampendi, taabu za ulimwengu,
    kwa nini mwaogopa kujitayarisha
    Kupokea kifo,
    kusudi muiage dunia mpokee raha ya milele
  5. Tofautisheni, kifo nayo mauti,
    mauti humpeleka mwenzetu kuzimu
    Ingawaje kifo,
    humtenganisha mwenzetu na taabu za dunia hii