Upendo na Ukarimu
Upendo na Ukarimu |
---|
Performed by | - |
Category | Love |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 4,834 |
Upendo na Ukarimu Lyrics
- Watu wengi tunajaribu upendo
Tunawajali wale wanaotuhusu
Tunaojua wataweza kutulipa
Hatuwathamini wale wasiotuhusu
Wala wasiojiweza, lakini
{Leo tumejifunza wote,
upendo ni kitu gani (wapendwa)
Tena tumepewa mfano,
ukarimu una sifa gani (wapenzi) } * 2
- Tunawakopesha wenye kipato kikubwa
Tukiamini nao watatukopesha
Wakitujia wenye shida na fukara
Tunawakimbia eti hawakopesheki
Na wana madeni mengi, lakini
- Wakiugua wenye nafasi za juu
Tunajazana kwao na vichupachupa
Tukiamini na sisi tukiugua
Watalundikana kwetu na vifuko fuko
Kadi na michango mingi, lakini
- Tukitembelewa na mtu mwenye viraka
Tunauliza kama tulimualika
Akija aliyeshuka kwenye shangingi
Tunamwuliza kinywaji anachokunywa
Tena kwa unyenyekevu lakini