Wamnunia Mungu

Wamnunia Mungu
Performed by-
AlbumIkulu ya Mbinguni
CategoryTBA
ComposerE. A. Minja
Views2,702

Wamnunia Mungu Lyrics

WAMNUNIA MUNGU

  1. Twajiuliza ewe ndugu yangu kwa kuyatafakari maisha yako
    Mawazo hata kwa matendo yako kila siku
    Upendo kwako kitu gani, amani moyoni i wapi
    Si kwa maneno hata kwa matendo upendo kwako umetoweka
  2. Daima wewe wa huzuni furaha imekukimbia
    Huzuni kwako meshika hatamu, furaha ya moyowe i wapi
    Kunapokucha ni kununa, mchana kutwa ni kununa
    Giza lijapo, na mwisho wa mwezi moyo wako hauna furaha
  3. Unapojiwa na mgeni, ndugu yako au rafiki hata jirani
    Hakuna wa heri, karibu kwako masikitiko
    Kwa mwenye jema kwako, unywe lenye baraka kwako
    Shida shukrani yako, tena wanuna sasa unamnunia Mungu
  4. Upatapo wanung'unika, ukosapo walalamika
    Bidii ya kazi imekutoweka, lipi kwako linakuridhisha
    Mwenzako anapokosea kauli kali wazipenda,
    Lugha nyeusi nazo wazipenda na hiyo ndiyo furaha yako
  5. Wivu ndiye rafiki yako, dharau ndilo gari lako
    Shambani mwako umepanda chuki sasa unavuna ubinafsi
    Moyo wako umeulinda kwa kuuwekea uzuio
    Uliojengwa kwa mawe magumu yaliyojengwa naye shetani
  6. maisha gani haya ndugu yasiyokuwa na upendo
    Yasiyokuwa hata na baraka kutokana na matendo yako
    Jitafakari ndugu yangu mwenendo wako ubadili
    Hebu jirudi kwa maisha haya au umeagana na Mungu