Tawi Limechipuka
Tawi Limechipuka | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Noeli (Christmas Carols) |
Views | 3,872 |
Tawi Limechipuka Lyrics
- Tawi limechipuka shinani mwa Yesu
Kama tulivyopashwa habari na wazee
Likatoa ua, wakati wa usiku, lililochanua - Isaya alitaja ua hilo zuri
Ni Yesu mponya wetu, Maria alimzaa
Usiku mtulivu, uwezo wake Mungu, umefanya hivi - Na ua hili dogo lanuka vizuri
Lang'aa kama jua, giza lafukuza
Ni Mwana wa Mungu, hata mwana Adamu, Mwokozi wa watu - Siku ya kufa kwetu, Yesu tuongoze
Tuiache dunia, twende furahani
Mbinguni kwa Mungu, pale tutakusifu, milele daima