Ni Ufalme
| Ni Ufalme |
|---|
| Performed by | - |
| Category | TBA |
| Views | 3,281 |
Ni Ufalme Lyrics
Ni ufalme wa utukufu wako anapotawala
watakatifu pamoja na Kristu wakivaa mavazi meupe
Wakimfuata Mwanakondoo popote aendapo
- Heri walio maskini wa roho
Kwa maana ufalme wa Mbinguni ni wao
- Heri walio wapole
Maana hao watairidhi nchi
- Heri wenye njaa na kiu ya haki
Maana watashibishwa
- Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki
Maana ufalme wa Mbinguni ni wao
- Heri wenye moyo safi
Maana hao watamuona Mungu
- Heri wenye huzuni
Maana hao watafairijiwa
- Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu
Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina