Ni Kweli Amezaliwa
Ni Kweli Amezaliwa Lyrics
Ni kweli amezaliwa Mkombozi wetu Masiha
Malaika wanaimba kwa furaha wakimsifu Bwana
{Na sisi tunafurahia Mkombozi wetu kazaliwa
Na utumwa umetutoka aleluya tushangilie } *2
- Kwenye mji wa Daudi Mkombozi kazaliwa
Wote twende tukamwone amelazwa manyasini
- Tuna haki kufurahi tumepata Mkombozi
Amekuja tukomboa hivyo wote tufurahi
- Utukufu juu Mbinguni, na amani duniani
Kwa watu wote wenye mapenzi mema aleluya
- Bwana Yesu kazaliwa, amekuja tukomboa
Katuletea wokovu, hivyo tuimbe aleluya