Siku Nzuri Kuna Nini
Siku Nzuri Kuna Nini Lyrics
- Siku nzuri kuna nini duniani watu wote
Duniani watu wote leo shangwe
Mnieleze leo shangwe ya nini
Mnieleze leo shangwe ya nini
- Siku nzuri kuna nini na kelele za vifijo
Na kelele za vifijo zasikika
Mnieleze leo shangwe ya nini
Mnieleze leo shangwe ya nini
- Ni furaha tele, na sherehe kubwa
Ulimwengu, umefanya sherehe kubwa
Mbinguni malaika wanaimba nyimbo nzuri
Tamu za kupendeza, twende tukaona
- Kuna nini pangoni Bethlehemu,
Kazaliwa mtoto mzuri mpole na mnyenyekevu
Twende tumsalimu
- Huyu mtoto ndiye Mwana wa Mungu
Huyu mtoto ndiye Yesu Kristu
- Ni Yesu Kristu, amekuja kwetu, amekuja kutukomboa sisi
Kweli ni furaha kubwa mno
- Ni Yesu Kristu, amekuja kwetu, amekuja kutukomboa sisi
Kweli ni furaha kubwa mno
- Tuimbe aleluya leo, tuimbe aleluya leo
Tuimbe aleluya leo, tuimbe kazaliwa Bwana
Aleluya tuimbe kazaliwa Bwana
- Ulimwengu, umefanya sherehe kubwa
Mbinguni malaika wanaimba nyimbo nzuri
Tamu za kupendeza, twende tukaona
- Kuna nini pangoni Bethelehemu,
Kazaliwa mtoto mzuri mpole na mnyenyekevu
twende tumsalimu