Kazaliwa Mtoto Mungu
Kazaliwa Mtoto Mungu | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Noeli (Christmas Carols) |
Views | 3,847 |
Kazaliwa Mtoto Mungu Lyrics
Kazaliwa mtoto Mungu, binadamu wote furahini
Kazaliwa Mtoto Mungu, umwendee wimbo wangu- Tangu elfu nne miaka
walimwagua manabii
Tangu elfu nne miaka
twamngojea na kumtaka - Ni mzuri, ni mpendelevu,
kitoto hicho Mwana mpenzi,
Ni mzuri, ni mpendelevu,
mwenye adhama, mtukufu - Banda la wanyama nyumbaye,
Kitanda chake ni manyasi
Banda la mnyama nyumbaye
Kwa Mungu hali gani je? - Atakaye nyoyo zetu
Zikae naye urafiki
Atakaye nyoyo zetu
Mara moja tumtoe tu