Sifuni Sifuni
Sifuni Sifuni Lyrics
- Sifuni sifuni
Upendo wake Mungu
Pazeni, pazeni enyi wa ulimwengu
Sifa zake bwan zifike kwa jirani
Hii ndiyo amani kwa wote duniani
Utabiri wa kale umetimizwa
Mungu ametujalia tulivyonenwa
Dunia yote imefurahi sana
Amezaliwa ndiye Mungu mwana
- Imbeni imbeni
Nyimbo za kushukuru
Semeni, semeni tumepewa uhuru
Wote yatupasa kuwa nayo furaha
Kuanzia sasa tujazwe uafasaha
- Mbinguni, Mbinguni
Wanaimba amani
Amani Amani iwepo duniani
Kwa watu popote aliowaridhia
Njooni na mpate alivyowaandalia
- Haya tazameni
Tuimbe Hosanna
Jamani Jamani ametujia Bwana
Heko mamajuzi kwa kumsujudia
Vivyi hata sisi twende kumtumikia