Pangoni Bethlehemu
Pangoni Bethlehemu |
---|
Alt Title | Pangoni Betlehemu |
Performed by | - |
Category | TBA |
Composer | W. G. Mushi |
Views | 3,278 |
Pangoni Bethlehemu Lyrics
Pangoni Bethlehemu, kazaliwa Mwana wa Mungu *2
Tuimbe wote aleluya, aleluya, aleluya,
Aleluya, ni furaha Bwana kazaliwa
- Kazaliwa mtoto Masiha wetu, twende Bethlehemu tukamwabudu
- Kazaliwa mtoto ndiye mfalme wetu, aja na ufalme begani mwake
- Tulimsubiri sana huyo mfalme wetu, sasa ameshuka kutukomboa
- Malaika Mbinguni wanamsifu Bwana, nao wanaimba nyimbo zashangwe
- Nasi pia twendeni huko Bethlehemu, twende na zawadi tukamtolee