Hodi Ee Wachunga

Hodi Ee Wachunga
Performed bySt. Peter Oysterbay
AlbumNyimbo za Noeli
CategoryNoeli (Christmas Carols)
ComposerA. Liampawe
Views4,526

Hodi Ee Wachunga Lyrics

  1. {Hodi ee Wachunga, amkeni msiwe na woga,
    Amkeni upesi amkeni hima twende Bethlehem } *2

    {Tukamuone Mtoto, tumwimbie na nyimbo
    Tumpigie na ngoma, aleluya leo } *2

  2. Mwokozi kazaliwa, mjini mwa Daudi
    Twende tumwone, tukamsujudu
  3. Nyasi amelalia, jukumu la Maria
    Akimtunza Mtoto, Mkombozi wetu
  4. Wafalme wa dunia, wanajipangapanga
    Wanafanya ghasia, juu ya Masiya
  5. Tuimbe kwa furaha, na ngoma tumpigie
    Kwa furaha na shangwe, tuimbe aleluya