Malaika Kaleta Noeli
| Malaika Kaleta Noeli | |
|---|---|
| Performed by | St. Peter Oysterbay |
| Album | Nyimbo za Noeli |
| Category | Noeli (Christmas Carols) |
| Composer | (traditional) |
| Views | 6,919 |
Malaika Kaleta Noeli Lyrics
- Malaika kaleta Noeli ya kwanza,
Kwa wachunga kondoo katika makonde,
Bethlehemu wakawa walinzi wa zamu,
Wakaona usiku ajabu ya nuru{ Noeli, Noeli, Noeli, Noeli,
Yesu yu Mungu na binadamu } *2 - Wakaona mbinguni, mwangaza wa nyota,
Ing'aayo kwa mbali na masharikini,
Wakaenda upesi, walivyoambiwa.
Bethlehemu wamwone Mwokozi horini - Mashariki watoka wafalme watatu,
Mamajusi waliotafuta mfalme,
Wafuata hii nyota waliyoiona,
Wasipate kumkosa wanayemtafuta - Kiongozi ni nyota iliyowaleta
Hata mji wa Daudi alimozaliwa
Ikakaa mara moja isiendelee
Pale pale nyumbani alimo Mwokozi - Mamajusi walipoingia nyumbani
Wakapiga magoti kwa heshima kuu
Mara hiyo walipozifungua hazina
Manemane, uvumba, dhahabu, watoa - Basi sisi wakristu na tumsujudie
Tumhimidi Mwokozi, aliyeviumba
Vitu vyote mbinguni duniani na sisi
Na ametufia na kutukomboa
* St. Peter Osterbay
* St. Cecilia