Bwana Aliniambia
| Bwana Aliniambia |
|---|
| Performed by | - |
| Category | TBA |
| Composer | John Mgandu |
| Views | 3,775 |
Bwana Aliniambia Lyrics
{Bwana aliniambia, ndiwe mwanangu,
mimi leo nimekuzaa leo, nimekuzaa leo }* 2
- Wafalme wa dunia wanajipanga na wakuu,
Wanafanya shauri pamoja juu ya Masiha wake.
- Yeye anayeketi huko mbinguni anacheka,
Naye Bwana anawafanyia dhihaka hao wafalme.
- Bwana aliniambia ndiwe mwana wangu,
Mimi nimekuzaa leo, nimekuzaa leo.
- Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,
Kama mwanzo, sasa na siku zote milele amina.