Ni Furaha Tushangilieni

Ni Furaha Tushangilieni
Performed by-
CategoryNoeli (Christmas Carols)
Views3,202

Ni Furaha Tushangilieni Lyrics

  1. Ni furaha tushangilieni, kazaliwa
    Mwokozi Yesu ni furaha tele Bethlehem
    Ule utabiri uliosemwa na Isaiah umetimia

  2. Yesu Kristu mwana wa Mungu kazaliwa huko
    Bethlehem, Twende tukamwabudu, twende
  3. Kuzaliwa kwake Immanueli Bwana Kristu
    Ni kuonyesha Mungu ni mkarimu, kweli
  4. Twende tumwone mashariki na malaika
    Alionyesha mwokozi kazaliwa, wote
  5. Waumini tumwimbieni kwa furaha
    Tumshangilieni mfalme mwenye nguvu,, kweli
  6. Nyumbani mwa daudi katoka mwana mwenye
    uwezo, wa kifalme tushangilieni, wote