Moyo Wangu Wamwadhimisha Bwana
Moyo Wangu Wamwadhimisha Bwana |
---|
Performed by | - |
Category | Bikira Maria |
Views | 5,308 |
Moyo Wangu Wamwadhimisha Bwana Lyrics
Moyo wangu wa mwadhimisha Bwana
Roho yangu yamfurahia Mungu
- Ni kwa kuwa ameutazama
unyonge wa mjakazi wake
- Kwa maana tazama tokea sasa
Vizazi wataniita mbarikiwa
- Kwa kuwa amenitendea mambo makuu
Na jina lake takatifu kweli
- Ameyatenda maajabu
na jina lake takatifu
- Wamchao hudumisha rehema
Vizazi hata na vizazi
- Amefanya nguvu kwa mkono wake
Atawanya wote wenye kiburi
- Aangusha wakuu wa enzi
Na wanyonge yeye huwakweza
- Wenye njaa amewashibisha mema
Walio na mali aondoa tupu
- Amemsaidia mtumishi wake
Ili kukumbuka rehema zake
- Utukufu kwao Baba na Mwana
Msaada wa Roho Mtakatifu
- Kama ulivyokuwa hapo mwanzo
Ni vivyo sasa hata milele
- Utukufu kwa Baba na Mwana kwa Roho
Kama vile mwanzo wa hata milele Amina