Litukuzeni Jina
Litukuzeni Jina Lyrics
- Litukuzeni Jina la Mungu daima milele
Enyi mataifa, mshangilieni Mungu wetu
Kwa kuwa Bwana ni Mtukufu wa kutisha
Yeye ni mfalme mkuu wa dunia yote
Sifuni Bwana kwa shangwe
{Jina la Mungu lihimidiwe daima milele
( litukuzwe litukuzwe litukuzwe litukuzwe litukuzwe litukuzwe)
Enyi mataifa mhimidini
Kwa kuwa fadhili zake (kwetu sisi) zadumu daima milele } *2
- Jina lake Bwana litukuzwe sasa hata milele
Viumbe vya Bwana Sifuni Bwana Mungu wetu
Toka mawio hata machweo ya jua
Sifuni jina lake Bwana Mungu wetu
Sifuni Bwana Mwenyezi
- Enyi watumishi sifuni Bwana kutoka Mbinguni
Mbingu nanyi maji, lisifuni jina la Bwana
Wafalme wa dunia nanyi watu wote
Wakuu nanyi wakaazi wote wa dunia
Sifuni Bwana Mwenyezi