Yesu Yupo
| Yesu Yupo |
|---|
| Performed by | - |
| Category | TBA |
| Composer | Bernard Mukasa |
| Views | 3,510 |
Yesu Yupo Lyrics
Yakija mawimbi hata dhoruba ikizidi
Nakanyaga maji nasogea Bwana Yesu
Upepo mkali hata bahari ichafuke
Nakanyaga maji nasogea Bwana Yesu
- Ni yeye Yesu alitembea juu ya maji (sikia)
Akamuita Petro ashuke akamfuate
Na hata Petro alipojawa na wasiwasi (sikia)
Yesu akawa pamoja naye na kutulia
- Nami ninayaacha niyasafiri nayo (sikia)
Nashuka nikamfuate Yesu niende naye
Nijapopatwa na misukosuko katikati (sikia)
Sitateteleka kwani Yesu yu pamoja nami
- Nitayatimiza yote atakoyonipa
Yesu ni wangu nami ni wa Yesu najivunia