Ee Ndugu Peleka
| Ee Ndugu Peleka |
|---|
| Performed by | - |
| Category | TBA |
| Composer | V. B. Kanuti |
| Views | 2,291 |
Ee Ndugu Peleka Lyrics
Ee ndugu peleka talanta yako kwa Bwana
Kwani Mungu alikupatia kwa kiasi chako
Nawe mrudishie Bwana kama wale watumishi
Kama wale waliopewa talanta mbili na tano
- Kumbuka waliopewa talanta mbili na tano
Walileta mbili na tano faida
Bwana wao akawasifu kwa uaminifu wao
Akawapokelea nao akawakweza
- Kumbuka aliwapatia tunzo la ufalme
Kwa hao waaminifu kwa hayo machache
Nao wakapewa yaliyo makubwa kwa bwana wao
Na sisi tupeleke talanta zetu kwa Bwana
- Kumbuka Mungu alivyokupatia kwa wiki nzima
Atataka kufanya hesabu nawe
Ukumbuke kutoa hesabu kama wale wawili
Naye Bwana Mungu wako atakupokelea