Hazina ya Mvivu
Hazina ya Mvivu | |
---|---|
Performed by | St. Anna Old Maswa Bariadi Shinyanga |
Album | Ona Wanadamu wa Leo |
Category | Tafakari |
Composer | J. Matthias |
Views | 2,469 |
Hazina ya Mvivu Lyrics
Hazina ya Mvivu ni maneno ya uongo (na tena)
Furaha ya mvivu ni kugombanisha watu- Hawezi kulala kapata usingizi usiku
Usiku mzima hukodoa macho akiwaza
Kukipambazuka aende kwa nani kupiga umbeya - Asubuhi mapema huamka na kuvaa nguo
Hajafagia nyumba huyo huyo kwa jirani kaenda
Hodi jirani jirani naye karibu tupo unasemaje
Atapiga umbea hapo hadi chakula cha mchana ale - Akipitapita mitaani huwa amependeza
Salamu kwa watu utasema huyu ni mtu mwema
Kumbe ni muovu asiye kuwa na aibu kwa watu - Wenzake wanaamka mapema na kwenda kazini
Yeye akiamka huyo huyo safari kwenye pombe
Akishafika huko tazama anavyolewa wala hawazi
Familia yake itakula nini mchana na usiku