Kuimba ni Raha
| Kuimba ni Raha |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Utume wa Uimbaji |
| Composer | Bernard Mukasa |
| Views | 6,665 |
Kuimba ni Raha Lyrics
Ni raha ni raha kuimba ni raha
Kumwimbia Bwana
Ni raha ni raha kuimba ni raha
Kumwimbia Bwana
- Pazeni sauti wapendwa imbeni
Mtatambua ilivyo raha
Tangazeni sifa za Bwana popote,
Ni baraka na ni raha sana jamani
- Sauti zetu zikifika kwa Mungu,
Malaika wataimba raha
Nazo zikimpendeza atashusha,
Heri neema na raha sana jamaani
- Tukimwimbia kwenye shida na tabu
Anatuhurumia sana
Kwenye huzuni ataleta faraja
Nguvu amani na raha sana jamani
- Kwenye mafanikio tunayopata
Tumshukuru kwa nyimbo Bwana
Atazidisha baraka zake kwetu
Tudumu katika raha sana jamani