Wimbo Mkuu

Wimbo Mkuu
Performed bySt. Yuda Thadei Mbeya
AlbumMlipuko wa Sifa
CategoryUtume wa Uimbaji
ComposerBernard Mukasa
Views8,112

Wimbo Mkuu Lyrics

  • Kwa zaburi, kwa zaburi, kwa furaha, kwa furaha
    Tunaimba, tunaimba wimbo mtamu, wimbo mzuri
    Kwa sababu wastahili kushangiliwa ewe Mfalme pokea wimbo mkuu
  • Kwa vinanda, kwa vinanda, na vinubi, na vinubi
    Tunaimba, tunaimba tenzi tamu, tenzi safi
    Kwa sababu wastahili kushangiliwa ewe Mfalme pokea wimbo mkuu
  • Mababu zetu waliimba, na wakaturithisha kuimba
    Kuimba (kuimba), kusifu (masifu), kusifu asubuhi na jioni sifa
    Masifu, sifa, sifa, sifa heshima nao utukufu kwako wewe
  • Tunakuimbia wimbo mkuu tukiwa chini tunaimba
    Ulimwenguni tunaimba, udhaifuni tunaimba
    Mbinguni juu malaika nao wanaimba wimbo mkuu
    Wimbo mkuu waimba aaa aaa aaaaaaaaaaaa
    aah aaa wanaimba ooo ooo ooo malaika wanaimba
    Mbinguni na watakatifu wanaimba,
    Ni raha sana kuimba wimbo mkuu
    Ni juu kwa wabarikiwa nao wasafi sana waimba wimbo mkuu
  • Tujaze nguvu tukuimbie, utuongoze tusiregee
    Yote yakatishayo tamaa yafukuze mbali yaondoke
    Tamaa yetu tukuimbie na binadamu ulimwenguni
    Mwisho tuimbe na malaika milele Mbinguni wimbo mkuu
  • Watu wote duniani wasikie
    Malaika wote wasikie
    Na watakatifu wote wasikie
    Na wakuimbie kwa sauti tamu
    Wanyama na ndege wote wasikie
    Bahari na vyote pia wasikie
    Nyakati zote wote wasikie
    Twakuimbia wimbo mkuu