Mungu Wangu Mungu Wangu Mbona Umeniacha
| Mungu Wangu Mungu Wangu Mbona Umeniacha | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Views | 10,754 | 
Mungu Wangu Mungu Wangu Mbona Umeniacha Lyrics
- Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha
- Wote wanionao huncheka sana
 Hunifyonya watikisa vichwa vyao husema
 hutegemea Bwana na amponye
 Na amwokoe sasa maana apendezwa na yeye
- Kwa maana mbwa wamenizunguka
 Kusanyiko la waovu wamenisonga
 Yamenizua mikono na miguu
 Naweza kuihesabu mifupa
- Wanagawanya nguo zangu
 Na vazi wanalipigia kura
 Nawe usiwe mbali
 Ee Mungu wangu fanya haraka kunisaidia
- Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu
 Katikati ya kusanyiko nitakusifu
 Ninyi mnaomcha Bwana, msifuni
 Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo mtukuzeni.
 
  
         
                            