Mshinda Nguvu za Shetani
Mshinda Nguvu za Shetani | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Pasaka (Easter) |
Views | 3,049 |
Mshinda Nguvu za Shetani Lyrics
- Mshinda nguvu za Shetani, Yesu kapaa Mbinguni
Malaika wake pia, wakaja kumshangilia - Tupe Yesu neema yako, tupate kufika kwako
Tufae sifu milele, wema wako juu kule - Umeshuka chini kwetu kuondoa dhambi zetu
Ukapaa kwake Mungu, utufungulie Mbingu - Ee Yesu wetu mkombozi, uwe wetu kiongozi
Uwe leo kitulizo, uwe kesho letu tuzo