Bwana Amepaa Mbinguni
Bwana Amepaa Mbinguni | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Kupaa kwa Bwana (Ascension) |
Views | 5,715 |
Bwana Amepaa Mbinguni Lyrics
Bwana amepaa Mbinguni aleluya (kweli)
Bwana amepaa kwa shangwe aleluya- Ninapaa kwenda kwa Baba yangu na Baba yenu
Kwa Mungu wangu na Mungu wenu - Mioyo yenu isihuzunike
kwa maana ninakwenda kwa Baba - Ninakwenda uwatengezea mahali
Nitakwenda tena kuwachukua - Ili mpate kuwapo
nilipo mimi - Kutoka Mbinguni, atakuja Mwokozi tunayemtazamia
Ndiye Bwana Yesu Kristu - Bwana atageuza, miili yetu ya unyonge
Upate kufanana na mwili wake na utukufu - Kristu alikufa
kwa ajili yetu akafufuka - Amekaa kuume kwa Baba
Ndiye anaye tuombea