Yesu Mwana wa Mungu

Yesu Mwana wa Mungu
Performed by-
CategoryPasaka (Easter)
Composer(traditional)
Views10,681

Yesu Mwana wa Mungu Lyrics

  1. Yesu Mwana wa Mungu * 2 Leo amefufuka
    Piga vigelegele *2 leo amefufuka

  2. Yesu Mwana wa Mungu kweli amefufuka
    Ahadi yatimia mzima amefufuka
  3. Kristu mshindaji, mkubwa ametupatanisha
    Na babaye Mbingunikwa damuye azizi

    Kristu mwanakondoo amechinjwa sadaka
    Tuile karamuye tuimbe aleluya
  4. Kristu mchingaji mwema alitoa maisha
    Kwa ajili ya kondoo mzima amefufuka
  5. Kristu aliuawa katika udhaifu
    Anaishi daima kwa nguvu yake Mungu
  6. Nendeni duniani kahubiri Injili
    Wote wabatizwao Mbingu watauridhi
  7. Nitawahubiria ndugu zangu daima
    Jina lako tukufu nitakusifu sana
  8. Leo ndiyo siku kuu ilifanywa na Mungu
    Umefufuka Mbingu kwa ushindi wa Yesu