Kwa Sherehe na Shukrani
   
    
     
         
          
            Kwa Sherehe na Shukrani Lyrics
 
             
            
- Kwa sherehe na shukrani ya moyo,
 wakristu leo tufanye shangwe
 Tumwimbie Mwokozi siku hiyo,
 amefufuka tufurahiwe
 Amefufuka asifiwe,
 tukaokoke kwa ufufuko we
- Maria Salome na Magdalene
 kaburini wenda alfajiri
 Nayo manukato na manemane
 kumtia Yesu kama desturi
- Mlangoni mwa kaburi wakifika,
 walikuta ndani yake wazi
 Waambiwa mara na malaika,
 hamo amefufuka Mkombozi
- Yesu u mfano wangu maishani,
 nipendelee utakatifu
 Nitatoka nami mzima kaburini,
 nitafufuka mwenye utukufu