Tuna Haki Kufurahiwa
Tuna Haki Kufurahiwa |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Views | 2,360 |
Tuna Haki Kufurahiwa Lyrics
- Tuna haki kufurahiwa leo, manabii walivyoagua
Yatimia sawasawa na chuo Rabi yetu amejifufua
- Mayahudi husema kwa kiburi amekwisha, juzi tukamwua
Kaburile limetimiwa mhuri, jiwe zito hapana fungua
- Mambo gani niambie Yahudi, Askari mbio wakimbia
Wana woga hao mjini warudi, kaza jiwe mhuri mpya tia
- Yahudi we, bure mashauriyo, sawa mshale urushwao juu
Ukianguka afumwaye ni huyo, za kupata hila zako kuu
- Mpumbafu we na Mungu kushindana, ukiwaza kumfunga kwa jiwe
Kaburini Rabi hayumo tena, iwo iwo kaamka mwenyewe
- Rabi yangu kweli amefufuka, na hakika ya imani yangu
Nayo basi kwa Yahudi kushtuka, mfumba domo, kimya kwa uchungu