Tuna Haki Kufurahiwa Lyrics

TUNA HAKI KUFURAHIWA

 1. Tuna haki kufurahiwa leo, manabii walivyoagua
  Yatimia sawasawa na chuo Rabi yetu amejifufua
 2. Mayahudi husema kwa kiburi amekwisha, juzi tukamwua
  Kaburile limetimiwa mhuri, jiwe zito hapana fungua
 3. Mambo gani niambie Yahudi, Askari mbio wakimbia
  Wana woga hao mjini warudi, kaza jiwe mhuri mpya tia
 4. Yahudi we, bure mashauriyo, sawa mshale urushwao juu
  Ukianguka afumwaye ni huyo, za kupata hila zako kuu
 5. Mpumbafu we na Mungu kushindana, ukiwaza kumfunga kwa jiwe
  Kaburini Rabi hayumo tena, iwo iwo kaamka mwenyewe
 6. Rabi yangu kweli amefufuka, na hakika ya imani yangu
  Nayo basi kwa Yahudi kushtuka, mfumba domo, kimya kwa uchungu
Tuna Haki Kufurahiwa
CATEGORYTafakari
SOURCETanzania
 • Comments