Rabi Yesu ni Mzima
Rabi Yesu ni Mzima Lyrics
- Rabi Yesu ni mzima leo na mapema akafufuka mzima
Rabi Yesu ni mzima si kaburini ni salama
Dhambini haoni, tu maskini, tu utumwani
Katuokoa motoni mwovu shetani mtafuta shani
Adui kashindwa haponi
- Za Rabi zetu nyimbo, twatia mapambo tusifu mambo
Za Rabi zetu nyimbo, ya shetani huvunja mitambo
Msalabani we, tuokolowe, Mungu mwenyewe
Hanyimi afungiwe, nasi wenyewe na moyo tuwe
haya tufuate mfanowe
- Rabi mshangilieni, watu wa imani, ndugu zangu karibuni,
Rabi Mshangilieni, ameshinda msiche shetani
Nasi hakika hapana shaka, tutafufuka
kaburi tutatoka, na malaika kuhesabika
Wema wa Mungu katuzika
- Mkate ukigeuka, Rabi atashuka, nyoyo zetu kutaka
Mkate ukigeuka, heshima twende kupeleka,
Na ninyi tena, taabu mkiona jueni vyema, leo raha hakuna
Tupande sana, kesho kuvuna,
milele na Rabi kuonana